<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Tazameni Huyo Ndiye TZR97</title>
<lyrics>[V1]
 Tazameni huyo ndiye,
 Mwenye kushinda vita;
 Haya, tumsujudie;
 Nyara anazileta;
 Watu wote msifuni,
 Sasa yumo kitini.

[V2]
 Msifuni malaika,
 Mtukuzeni sana,
 Wote waliookoka
 Watamsifu Bwana;
 Watu wote msifuni,
 Sasa yumo kitini.

[V3]
 Walimfanya dhihaka
 Zamani wenye shari,
 Kwao waliookoka
 Ni Bwana wa fahari;
 Watu wote msifuni.
 Sasa yumo Kitini.

[V4]
 Nyimbo nzuri, sikizeni,
 Ni nyimbo za sifa kuu,
 Za Bwana Yesu kitini,
 Kutawazwa, yeye tu;
 Watu wote msifuni
 Sasa yumo Kitini.</lyrics>
<hymn_number>97</hymn_number>
</song>